Saturday, April 18, 2015

WAHAMIAJI HARAMU WAKUTWA WAMEFICHWA KWENYE FUSO LILILOBEBA TOILET PAPER ENEO LA CHANGBAY MOSHI......LILIGAWANYWA SEHEMU 2, NYUMA TOILET PAPER NA KATI WAHAMIAJI LIKIWA LIMEFUNGWA TURUBAI

POLISI mkoani Kilimanjaro inawashikilia wahamiaji haramu 52 ambao ni raia wa Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria wakitokea Kenya kwenda Malawi na baadaye Afrika Kusini.

Wahamiaji hao waliokamatwa jana saa 8.23 za asubuhi wakati askari wakiwa doria katika eneo la Changbay, barabara kuu ya Moshi ña Arusha
wilayani Moshi, walikuwa raia 44 wa Ethiopia.
Kamanda Polisi mkoani hapa, Geofrey Kamwela, alisema raia hao walikuwa wakisafirishwa kwenye gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T209 BVL, ambapo lilikuwa limepakia karatasi cha matumizi ya chooni maarufu kama toilet paper ambalo lilikuwa likiendeshwa na Elisha Manyani (45).

Mtu huyo alikamatwa na wenzake watatu ambao Hamza Ali (24), Isaya Patrick (25) na Steven Swame(39) wote wakazi wa Arusha.

ìWahamiaji hao walikuwa wamepakizwa kwenye gari aina ya Fuso, ambapo katika gari hiyo, bodi ilikuwa imegawanywa sehemu mbili nyuma kulikuwa kumewekwa toilet paper na katikati palikuwa pamewekwa raia hao likiwa limefungwa turubai, jambo ambalo lilikuwa gumu kubaini kama ndani kuna raia hao,îalisema Kamwela.

Alisema majira ya 8.45 asubuhi raia wengine wanane walitiwa mbaroni katika eneo la eneo la KDC kwenye Kata ya Kiboroloni, ambapo walikutwa wakizagaa katika pori dogo karibu na mto Rau.

Kamanda alisema wanaendelea na uchunguzi na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watuhumiwa hao.
Hatutawafumbia macho raia hao wa Kitanzania wanaoshirikiana katika kusafirisha wahamiaji haramu na hatua kali za kisheria zitachukuliwa na hata kutaifisha mali zao pindi watakapokutwa na hatia,” alisema.

UHURU ONLINE

No comments:

Post a Comment