Jaji mmoja nchini Argentina ametoa agizo la kukamatwa kwa
mwanamuziki Justin Bieber siku ya ijumaa akisema kuwa mwimbaji huyo alikataa
kufika mbele yake kuhusiana na madai kwamba aliwaagiza walinzi wake
kumshambulia mpiga picha mmoja mwaka 2013.
Jaji Alberto Julio Banos aliagiza kukamatwa kwa Bieber na
walinzi wake Hugo Alcides Hesny na Terrence Reche Smalls.
Ujumbe uliotumwa kwa Bieber haukujibiwa mara moja.
Bieber anashtumiwa kwa kuwatuma walinzi hao kumshambulia
mpiga picha Diego Pesoa nje ya kilabu moja ya Bueno Aires.
Msanii huyo hatahivyo hakurudi nchini Argentina ili
kujibu maswali kuhusu kisa hicho.
Chini ya sheria za Argentina Bieber atakabiliwa na kifungo
cha kuanzia mwezi mmoja hadi miaka sita jela iwapo atapatikana na hatia ya
shtaka la kumjeruhi mpiga picha huyo.
BBC
No comments:
Post a Comment