Meneja Uhusiano wa TANESCO, Adrian Severin |
Imeelezwa kuwa mfumo unaotumika sasa ni tatizo
kutokana na mabadiliko hayo, mfumo mpya huenda ukaanza kutumika mwezi ujao.
Hayo yalisemwa jana na Meneja Uhusiano wa Tanesco, Adrian Severin.
Alisema mfumo utakaowekwa, utakuwa wa kisasa na
kwamba utawasaidia watumiaji kupata haraka huduma ya Luku. Alisema mfumo huo ni
wa kompyuta, wa kisasa na wa haraka, utakaotibu kero wanayoipata watumiaji wa
huduma ya Luku.
‘’Mfumo huo utakuwa una uwezo wa kuhudumia
wateja wengi zaidi na kwa haraka ndani ya sekunde tatu, ikilinganishwa na mfumo
wa zamani ambao ulikuwa unatumia zaidi ya dakika moja au sekunde 30,’’ alisema
Severin.
Aliongeza maandalizi ya mfumo huo, yamekamilika
na kwamba watakaokuwa wanatumia simu za mikononi na mawakala wanaouza Luku,
wataendelea kutoa huduma hiyo.
‘’Mawakala wa MaxMalipo na simu zote za mikononi
kama Tigo, Airtel, Zantel na Vodacom wataendelea kutoa huduma hiyo, lakini
itakuwa kwa haraka na kwamba hakutakuwa na shida ya mitandao,’’
alisema.
Akizungumzia suala la kutopatikana kwa huduma ya
Luku tangu juzi jioni, Severin alisema huduma hiyo haikupatikana, kutokana na
tatizo la mtandao.
‘’Wakati mwingine simu za mikononi zinakuwa
hazina tatizo la mitandao, lakini unakuta Tanesco mitandao yao ipo chini, vivyo
hivyo na kwamba Tanesco inakuwa ipo sawa kwa mtandao, lakini simu zinasumbua,’’
alisema Severin.
Alisisitiza kuwa ili kupatikana haraka kwa
huduma ya Luku, inatakiwa Tanesco na simu zote zinazotoa huduma hiyo kuwa na
mitandao iliyo sawa. Hata hivyo, alisema huduma hiyo inapatikana kwa
sasa.
Kwa muda mrefu, watumiaji wa huduma ya Luku,
wamekuwa wakilalamikia uduni wa huduma, kiasi cha kuwafanya wateja wake
kushindwa kuwa na umeme kwa siku kadhaa, kutokana na tatizo la kimfumo katika mitambo
ya huduma za Luku.
Chanzo: Habari Leo
No comments:
Post a Comment