Msanii wa Bongo Fleva,Hussein Machozi amefunguka na
kusikitishwa na habari zilizoenea kuwa amefariki dunia baada ya kupata ajali ya
gari mkoani Dodoma.
Alisema kuwa tangu habari hizo kuenea siku ya jana
amekuwa akipigiwa sana simu na watu tofautitofauti wakimuuliza kama mzima wa
afya. ‘’Jana nilikuwa
nimezima simu kwa muda mrefu nilikuwa nimeenda mazoezini
baada ya kurudi nilipowasha tu simu ziliingia kama mvua kilichonishangaza wengi
walikuwa wakipiga wakisikia sauti yangu wanakata simu,’’alisema Hussein
Machozi.
‘’Yaani kuna watu wamenipigia simu ambao walikuwa walishakata
mawasiliano na mimi muda mrefu na nimeambiwa nyimbo zangu zimepigwa sana siku
ya jana baada ya taarifa hiyo kuzagaa,’’aliongeza Hussein Machozi.
Aidha aliongeza kuwa ameamini kuwa msanii akishakufa
thamani yake inaongezeka sana,na anatarajia kufanya dua na kualika watu
mbalimbali nyumbani kwao kwa ajili ya kujiombea kutokana na tukio hilo.
CloudsFM
No comments:
Post a Comment