WATUMIAJI wa mitandao ya kijamii nchini wametakiwa
kujiandaa kutumia sheria mpya ya mawasiliano iliyopitishwa bungeni hivi
karibuni.
Akizungumza na kituo cha redio cha Clouds, Dar es Salaam
jana, Meneja Mawasiliano wa
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent
Mungy alisema kuwa kila mtu anatakiwa kutambua kuwa anawajibika katika matumizi
ya mawasiliano.
Mungy alisema TCRA kwa kushirikiana na serikali,
wataiweka sheria hiyo kwenye mitandao na kwamba kila mmoja anapaswa kuisoma na
kuielewa.
Pia alisema wanajiandaa kutoa elimu kuhusu sheria hiyo na
jinsi watumiaji wa mitandao ya kijamii wanavyopaswa kujihadhari ili wasije
kuwajibika.
No comments:
Post a Comment