MAHAKAMA ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma imempa adhabu
ya kufua mashuka ya wagonjwa katika hospital ya Wilaya ya Kakonko na kuzibua mitaro ya barabarani Diwani wa
kata ya Kasanda kupitia tiketi ya chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yeye na wenzake wanne kwa muda wa siku
kumi na nne baada ya kukutwa na hatia ya makosa matatu.
Mwendesha mashtaka alisema kuwa mnamo novemba 8 mwaka
jana majira ya saa kumi jioni katika kijiji cha kaziramihunda watuhumiwa wote
kwa pamoja walifika katika ofisi ya Ofisa mtendaji wa kijiji hicho isivyo
halali na kuifunga ofisi hiyo kwa kuweka gundi aina ya super gluu na unga wa
ngano kwenye kufuli ili kumzuia mtendaji asifanye kazi yake.
Inadaiwa kuwa watu hao walifikia uamuzi huo kwa madai
kuwa hawamtaki mtendaji huyo wa kijiji Amos Peter na kumtishia kuwa watamuua.
Kufuatia hali hiyo Diwani huyo na
wenzake,Mahakama ya
Wilaya ya Kibondo imewahukumu kulipa faini ya shilingi elf 50 au kufungwa jela
miezi mitano kwa kosa la kufunga ofisi ya mtendaji,na pia kulipa faini ya
shilingi elf 50 au kwenda jela miezi miwili kwa kosa la kufanya fujo.
Watuhumiwa wote walilipa faini na kuachiwa huru isipo
kuwa Hatare Kasase(33)ambaye anakabiliwa na kesi nyingine ya mauaji hivo
alirudishwa gerezani.
Aidha katika kosa la kutishia kuua Diwani huyo na wenzake
watatu wamehukumiwa adhabu ya kazi za kijamii ambayo ni kufua mashuka ya
wagonjwa katika hospital ya Wilaya ya Kakonkokwa muda wa wiki moja na kuzibua
mitaro ya barabara kwa muda wa wiki moja pia.
Ambapo tayari wameshakabidhiwa katika idara ya maendeleo
ya jamii kwaajili ya kuanza adhabu hiyo.
Watuhumiwa wengine kayika kesi hiyo waliachiwa huru baada
ya kukutwa hawana hatia, waliochiwa huru ni Bonifasi Obadia(35)Amos
buseni(33)majaliwa Charles(24)pamoja na Samora Barichako(35)wote wakazi wa
kijiji cha kaziramihunda.
Chanzo: Michuzi
No comments:
Post a Comment