BABA NA MAMA WA HAO MAPACHA 5 |
Mapacha watano wa kike wamezaliwa Marekani katika
hospitali moja ya wanawake mjini Texas Houston.
Wauguzi katika hospitali hiyo wanasema kuwa uzazi huo
kutokana na mimba moja ni rekodi mpya
ambayo haijawahi kutokea Marekani.
Danielle Busby ambaye ndiye mama wa watoto hao ambao
wamepewa majina ya Olivia Marie, Ava Lane, Hazel Grace, Parker Kate na Riley
Paige;anasema kupata watoto hao wote wakiwa wazima kwake ni baraka ya hali ya
juu.
Inasemekana watoto wengi sawa na hao walihahi kuzaliwa
mara moja huko London Uingereza ,mwaka 1969 katika hospitali ya Queen
Charlotte.
Zaidi ya Madaktari na wauguzi 12 walilazimika kufanya
kazi ya ziada ilikumsaidia bi Busby kujifungua watoto hao ambao hawakuwa
wametimiza umri wa miezi tisa tumboni kwa njia ya upasuaji .
Baba wa mtoto huyo, Adam Busby amewamiminia sifa kedede
wahudumu wote wa hospitali hiyo waliofanikisha operesheni hiyo.
Bi. Busby alikuwa na tatizo la kupata ujauzito hivyo
akatumia mbegu pandikizi ya uzazi.
Bwana Busby amesema kuwa mwanawao wa kwanza Blayke
anawasubiri kwa hamu na ghamu.
Bi. Busby alikuwa na tatizo la kupata ujauzito hivyo
akatumia mbegu pandikizi ya uzazi kwa mimba zake zote mbili.
BBC
No comments:
Post a Comment