Iman Abdulmajid aliishi nchini Marekani kama mhamiaji
haramu.
Iman: Nilidanganya na kusema kuwa nilikuwa na umri wa
miaka 19 ili kupata pasipoti kwa kuwa bila hivyo ningelazimika kupata rukhsa
kutoka kwa wazazi wangu na wazazi wangu hawangeniruhusu mimi kwenda Marekani.
Mbali na kuidanganya serikali hiyo mwanamitindo huyo
mwenye umri wa miaka 60 pia aliwadanganya wazazi wake kwa makusudi kuhusu kule
aliko.
Iman alitarajiwa kuwa chuo kikuu cha Nairobi wakati
alipoelekea New York ,kwa hivyo alidhani kwamba wazazi wake hawatagundua kule
alikokwenda lakini baada ya mda mfupi baba yake alimuona katika gazeti la
Newsweek.
Akizungumza na Gazeti la New York,Iman alisema:Ni Gazeti
hilo analosoma baba yangu na alipokuwa akisoma aliona picha yangu na maandishi
kwamba ''ndiye mwanamitindo mrembo kwa sasa''.
Nilivunja sheria lakini hakuna mtu ambaye anaweza
kunishika hivi sasa, alijigamba mwanamke huyo.
No comments:
Post a Comment