MSANII wa Bongo Fleva, Nassib Abdul (Diamond Platnumz),
amesema ujauzito aliobeba Zarina Hassan ‘Zari’ anaona kama amewekwa kwenye
kiganja cha mchumba wake huyo.
Diamond alisema licha ya kutokuwa na fikra ya kuwa na
maisha ya kujenga familia na msichana huyo wa Uganda, ila ujauzito alionao
unaotarajiwa kumletea mtoto umekuwa chachu kubwa ya kuongeza mapenzi kwa Zari.
“Sikutegemea kuwa na Zari, lakini kwa hali aliyonayo sasa
ya ujauzito ni kama ameniweka kiganjani na sasa ninachoomba mtoto azaliwe
salama na awe na akili nyingi,’’ alisema Diamond.
Diamond aliongeza kwamba wasichana wengi aliowahi kuwa na
uhusiano nao walikosa vitu vya kufanana naye.
“Niliokuwa nao nadhani kulikuwa na vitu ambavyo
havikukamilika, ndiyo maana hatukuwa tukiishi kwa muda mrefu na kuanzisha
maisha kama haya na Zari,’’ alisema Diamond.
MTANZANIA
No comments:
Post a Comment