Muigizaji maarafu wa filamu nchini Tanzania,Wema Sepetu
alizomewa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram
baada ya kuweka picha ya mlimbwende Hamisa Obetto akiwa
mjamzito na kuandika maneno ya mshangao
”Jamani my mdogo umezaa.!wewe ni mwanamke sasa”.
Ujumbe huo ulizusha tafrani kwa baadhi ya watu na kumjibu
Wema kwa maneno makali yenye kebehi ya
kwa nini yeye hazai anakaa kushabikia watoto wa wenzie
tu.
Gumzo hilo lilifwata mkondo tofauti pale ambapo mchumba
wake wa zamani mwanamuziki Diamond Platinum
akitarajia kupata mtoto na bi.Zari kutoka Uganda ambaye
ni mpinzani wake mkubwa Wema.
Wema Sepetu aliweza kujibu tuhuma hizo kwa kusema yeye si
mpanga wa yote,''ningekuwa na uwezo wa kuzaa angezaa siku nyingi ila ni Mungu
ndiye anapanga'',
Alisema kuwa ''nimekuwa nikihangaika kupata mtoto usiku
na mchana''
aliongezea kusema kuwa si rahisi kwa yeye kuwaambia kila
kitu,kwani yeye pia ni binadamu na kuwa
''anaumia sana na maneno makali watu wanayoandika au
kusema kumhusu''.
Ujumbe wa simanzi kutoka kwa muigizaji huyo ulirudiwa na
baadhi ya waigizaji kama Iren Uwoya na mashabiki wengine
ukionya tabia ya watu kutoa matusi makali kwa Wema bila
kuangalia upande wa pili,maana siku hizi kuna team kwenye mtandao pia zikijiita
team Wema na Team Zari
BBC Swahili
No comments:
Post a Comment