Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa Hillary
Clinton atakuwa rais bora na mwenye maono kwa nchi ya Marekani. Bi Clinton
anatarajiwa kutangaza hii leo kuwa atawania uteuzi wa chama cha Democratic.
Obama amesema kuwa Bi Clinton alitekeleza kwa njia nzuri
majukumu yake alipohudumu kama waziri wa mashauri ya kigeni. Atatangaza azma
yake ya kuwania urais kwa njia ya video ambayo itasambazwa kupitia kwa mitandao
ya kijamii.
Kinyume na miaka minane iliyopita Bi Clinton anatarajiwa
kuangazia zaidi jinsi wapiga kura wataandikisha historia kwa kumchagua kuwa
mwanamke wa kwanza rais wa Marekani.
BBC
No comments:
Post a Comment