STAA wa filamu za kibongo, Wema Sepetu ‘Beautiful
Onyinye’, amesema ni ushamba kwa wasanii wa muziki kuwatungia nyimbo za majungu
wasichana wanaoachana nao kimapenzi.
Wema amesema wasanii wengi wa muziki wamekuwa na tabia ya
kishamba ya kutunga nyimbo zenye maneno ya kuudhi, wakiwalenga waliokuwa
wapenzi wao.
“Ni ushamba wa mapenzi, haiwezekani mlikuwa mnafurahia
wote mapenzi yenu, lakini mkiachana anakutungia nyimbo za kukuponda, hakuna
neno la kuzungumzia hilo zaidi ya kuita ushamba kwa wasanii wa aina hiyo,’’
alisema Wema.
Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo chetu cha ndani kutoka
studio moja kubwa ya kurekodi muziki nchini, kuna wimbo wa wasanii wawili
waliowahi kuimba pamoja na wimbo wao ukawa gumzo kwa mashabiki wa muziki huo,
ambao wanamalizia kurekodi wimbo unaodaiwa unamzungumzia mrembo huyo wa
Tanzania mwaka 2006.
MTANZANIA
No comments:
Post a Comment