BAADA ya mwigizaji Wema Sepetu kuweka wazi juu ya
masikitiko yake ya kutopata mtoto licha ya kumtafuta kwa muda mrefu, mwigizaji
mwingine wa Bongo Movie, Mayasa Mrisho ‘Maya’ naye ameibuka na kudai kwamba
anazeeka bila kupata mtoto.
Maya alisema wasanii wenzake wana watoto na wengine
wajawazito, lakini yeye bado hajabarikiwa kupata mtoto, jambo linalompa hofu ya
kuzeeka bila mtoto.
“Nazeeka bila mtoto wa kumzaa, hapa namuomba Mungu
aniwezeshe na kunifungulia uzazi niweze kupata motto, maana umri unakwenda,
nitazeeka bila ya kuwa na mtoto jamani,’’ alisikitika Maya.
Kutokana na kauli hiyo, Maya anakuwa mwigizaji wa pili
kuweka wazi ya moyoni mwake ya kutokuwa na mtoto na nguvu zao wamezielekeza
katika maombi.
MTANZANIA
No comments:
Post a Comment