Wazazi wenye watoto wadogo huwa wananiuliza kama inawezekana
kuwa na nyumba iliyopambwa vizuri na kuwa na watoto ndani wakati huohuo. Jibu
ninalowapa ni NDIO! Njia nne za kuweza kupamba nyumba yako hata kama unaishi na
watoto wadogo ni hizi.
Sehemu kubwa ambayo watoto wanapenda kucheza na kuchafua kwa
vyakula na vinywaji ni kwenye sofa. Hata kama utajitahidi kuwazuia namna gani
mwishoni hivyo vita mzazi hutaviweza, utashindwa tu, kwani utatoka na kurudi na
kukuta wameshamwaga tomato sauce. Suluhisho lake ni weka sofa zenye kitambaa
kisichoonyesha uchafu na pia vitambaa vyake viwe ni vya kuvulika kiasi kwamba
unaweza kuviondoa na kufua.
Usiweke coffee table ya kioo, weke ya mbao ambayo ncha zake
sio kali au kama utapenda nzuri zaidi ni ya kitambaa (ottoman). Coffee table ya
kioo ina uwezekano mkubwa wa kuvunjwa na watoto na ikawaumiza vilevile.
Ongeza mapambo kwenye zile sehemu ambazo watoto wako wadogo
hawafilkii. Unaweza ukawa na display cabinet lenye mapambo yako ya crystal na kwa
vile watoto hawafikii vikakaa vizuri kabisa, badala ya kuviweka juu ya coffee table.
Hata picha za ukutani zilizo juu watoto ambao hawajawa na uelewa hawawezi
kuzifikia
Watoto wanapenda kuvuta pazia na kujificha nyuma ya pazia.
Kwa kufanya hivi wanaweza kuzing’oa na pia kuzichafua. Suluhisho lake ni kuwa
ukiwa na watoto wadogo weka pazia fupi, zinazopita dirisha kidogo tu, usiweke
zile za kuburuza hadi sakafuni kwa kuwa zitakuwa kishawishi kwao kuzichezea.
Usikose kupita kesho kwa tip nyingine ya nyumbani….upate
siri za kufanya makazi yako yaonekane nadhifu.
No comments:
Post a Comment