Serikali ya Kenya inatoa zawadi ya dola 220,000 kwa
taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwa mwanachama wa kundi al-Shabab
aliyeshukiwa kuhusika mashambulizi katika mashambulizi ya Garissa Alhamisi
ambapo watu 147 waliuawa.
Mtu huyo, Mohammed Mahamoud Kuno,
ambae tayari yupo
kwenye orodha ya watu wanaotafutwa na serikali ya nchi hiyo anashukiwa kuwa
mkuu wa operesheni za nje wa kundi la al-Shabab dhidi ya Kenya. Pia anajulikana
kwa jina la Gamadhere au Dulyadayna.
Kuno anatafutwa ili aweze kuhojiwa kuhusu shambulizi
kwenye chuo kikuu cha Garissa mahala ambako washambuliaji walishambulia majengo
ya chuo alfajiri ya Alhamis na kufyatua risasi.
Viongozi wa kigeni wamelaani shambulizo hilo na rais wa
Somalia Hassan Sheikh Mohamud ametowa wito wa kuwepo na ushirikiano mkubwa
zaidi na kenya, alipotoa rambi rambi zake kwa wakenya.
Viongozi wa kigeni wamelaani shambulizo hilo na rais wa
Somalia Hassan Sheikh Mohamud ametowa wito wa kuwepo na ushirikiano mkubwa
Zaidi na kenya, alipotoa rambi rambi zake kwa wakenya.
Chanzo VOA
No comments:
Post a Comment