Serikali ya Kenya imetuma ujumbe katika mtandao wake wa
Twitter ikisema kuwa Watu 500 wameokolewa huku 70 wakiuawa wakiwemo wapiganaji
4 wa kundi la Alshabaab
Baadhi ya majeruhi ambao walisafirishwa kwa njia ya ndege
kutoka Garissa wamewasili ili kupata matibabu katika hospitali kuu ya Kenyatta
mjini Nairobi Kenya.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametuma risala za rambi
rambi kwa familia za wale waliouawa katika shambulizi la chuo kikuu cha Garissa
kazkazini mashariki mwa Kenya.
Kiongozi huyo vilevile amewahakikishia wakenya
kwamba serikali yake imechukua hatua za kuwapeleka maafisa wa usalama katika
eneo hilo.Amewataka wakenya kuwa watulivu wakatu huu ambapo maafisa wa usalama
wanakabiliana na wapiganaji hao
BBC Swahili
No comments:
Post a Comment