Mwanamama nguli na nyota wa kipindi cha runinga cha The
Keeping Up with the Kardashians,Kim West ambaye ana mtoto mwenye umri wa miezi
21 North West aliyezaa na mumewe Kanye West,imeelezwa na mumewe huyo Kanye
,mkewe hataki chochote katika ulimwengu huu zaidi ya kupata mtoto mwingine
,lakini madaktari wamemuonya anaweza kukabiliwa na hatari kiafya.
Katika kipande cha kipindi kinachofuata cha kipindi cha
mwanamama huyo ambacho kitarushwa katika runinga ya E’ inayojihusisha na
masuala ya burudani na huenda kipande hicho kitarushwa mwishoni mwa wiki hii
,kipande hicho kinamuonesha Kim akielezea alichoambiwa na daktari wake kuwa
anajaribu kumficha Kanye West anachotakiwa kwenda kufanyiwa na madaktari
kuondoa kitu kilichoko kwenye kizazi chake.
Na ilipobidi kumkabili mumewe huyo, ambaye ni nguli wa
muziki wa tambo,alipomwambia juu ya suala hilo tete, alikubaliana nalo na
kumwambia endapo atafanikiwa kupata mtoto wa pili atakuwa wa mwisho kwasababu
kondo la uzazi linakua kwenye kizazi chake.
Lakini baadaye mrembo huyo alionekana kukata tamaa ya
kupata mtoto mwingine,na akaeleza wazi kuwa alipokuwa mjamzito wa mtoto wao wa
sasa North,alikuwa akiwaambia watu wake wa karibu kwamba hakuna kiwango cha
pesa duniani atakachoweza kulipwa kurejea tena katika maumivu ya uchungu wa
kuzaa.
Lakini, kwasasa hakuna kitu ninachokihitaji zaidi
ulimwenguni kama kuwa mjamzito tena,nina pata hasira kidogo kwamba watoto wangu
wataachana miaka kadhaa.
Siku za karibuni Kim alitoa ya moyoni kwa kueleza kwamba
ulikuwa ni muujiza kuipata mimba ya mtoto wake North kwasababu madaktari
walisha mwambia kuwa milele hataweza kubeba ujauzito .
No comments:
Post a Comment