Katibu mkuu wa Wizara ya Tamisemi Jumanne Sagini. |
Serikali imeagiza Wakurugenzi wa halmshauri manispaa na
majiji kuwachukulia hatua walimu wakuu waliotangaza kufungwa kwa shule kutokana
na ukosefu wa chakula kwa kuwa hawakufuata taratibu.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaama Katibu mkuu wa
wizara ya TAMISEMI Jumanne Sagini amesema kuwa walimu hao hawakustahili
kutangaza kufungwa shule wangewasiliana na wakurugenzi ambao ndio wenye mamlaka
huku akisisitiza kuwa pesa tayari zilishapelekwa katika akaunti za
Halmashauri.
Akizungumzia kuhusu malipo ya wazabuni ambao wanadaiwa
kugomea kusambaza chakula kutokana na kutolipwa pesa zao amesema kuwa tangu
Julai Mwaka jana hadi Machi mwaka huu serikali imelipa zaidi sh bilioni 28.1
sawa na asilimia 66.7 ya madeni ya wazabuni.
Sagini amesema ameshangazwa na kusikia kuwa shule
zimefungwa kutokana na kukosa chakula wakati fedha zimeshapelekwa kwenye
halmashauri zao na kushangazwa na kusikia kuwa wazabuni hao hawajalipwa.
EATV
No comments:
Post a Comment