Mwanamuziki mkongwe Madonna amejijengea sifa ya kutokua
muoga katika maswala ya ngono wala ya kijamii.
Lakini alichokifanya mwishoni mwa juma liliwaacha wengi
vinywa wazi .
Bibi huyo mwenye umri wa miaka 56 alishindwa kustahimili
mvuto wa mwanamuziki wa kizazi kipya Drake alipokuwa akimwaga misstari mbele ya
mashabiki wake katika onyesho
la California Coachella.
Malkia huyo wa mziki wa ''POP'' alitua jukwaani Drake
alipokuwa akiimba wimbo wake maarufu ''Madonna''
ilionekana kama aliyeshikwa na jazba baada ya kushuhudia
wimbo wa ''Human Nature'' na ''Hung Up''
na akajipata jukwaani akampiga pambaja na kumkumbatia na
mara akampiga busu.
Drake hakusema lolote wakati huo lakini alionekana kama
aliyeshtuliwa sana na tukio hilo.
Drake baada ya kupigwa kubusu na Madonna
Picha zinaonesha alishikwa na kinyaa.
Ajabu nikuwa i Madonna alimpokonya kinasa sauti na kusema
"mimi ndiye Madonna" na akaondoka jukwaani.
BBC
No comments:
Post a Comment